Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashililah, akisalimiana na baadhi ya Wajumbe wa Kamati za bajeti na Fedha wa Bunge la Korea, waliofika kutembelea Ofisi hizo jijini Dar es Salaam leo mchana na kufanya mazungumzo ya jinsi ya kudumisha ushirikiano.
Wakiwa katika kikao hicho....cha pamoja...
Ofisa wa Itifaki wa Ofisi za Bunge nchini, Said Yacoub, akiwaongoza wajumbe hao kuingia kwenye Ofisi za Bunge Jijini Dar es Salaam leo mchana.
Na Sufianimafoto Reporter, Jijini
WAJUMBE wa kamati ya bajeti ya fedha wa bunge la Korea ya Kusini wamekutana na Katibu wa bunge la Tanzania Jijini Dar es Salaam jana na kufanya mazungumzo kwa lengo la kuendeleza ushirikiano uliokuwepo baina ya nchi hizo.
Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu lengo la mkutano huo, Ofisa wa Itifaki wa Ofisi za Bunge nchini, Said Yacoub, alisema kuwa wajumbe hao wamefika kutembelea ofisi za bunge ikiwa ni pamoja na kubadilishana uzoefu katika kazi na kudumisha ushirikiano.
Aidha yacoub alisema kuwa imekuwa ni kawaida kwa wabunge wa Korea kufika kujifunza kazi na kubadilisha uzoefu ambapo na wabunge wa nchini pia wamekuwa wakitembelea bunge la Korea kwa lengo hilo.
"Tumekuwa tukifanya kazi kwa pamoja kwa muda mrefu na hii pia imekuwa ni changamoto kwetu ya kurahisisha kupata misaada mbalimbali" alisema Yacoub.
Katika kikao hicho kilichowakilishwa na Katibu wa Bunge kwa niaba ya Spika, kilijadili kuhusu makubaliano mbalimbali yanayowahusu wafanyakazi wa bunge ambayo ni pamoja na semina za mafunzo kwa maafisa waandamizi juu ya utawala na kuendesha mafunzo ya usimamizi wa fedha kwa wahasibu na kufanya matemebezi katika kujifunza na kubadilishana mikakati kwa wajumbe katika kazi mbalimbali zinazohusu bunge.
Pia kilijadili umuhimu wa misingi bora ya bunge ambayo ni muhimu kwa sababu zinasaidia bunge kutatua mambo mbalimbali na kuwa imara zaidi katika kazi zake kama inavyojulikana kuwa bunge ni kiungo kwa Serikali, muhimu katika mawasiliano ya kutekeleza mahitaji ya wananchi kiurahisi.
Aidha alisema kuwa bunge lipo kwa niaba ya wananchi katika kuhakikisha uwazi na usimamzi wa mambo ya kiuchumi na sheria mbalimbali zinazohusu haki za binadamu.

No comments:
Post a Comment