
Baadhi ya warembo wa Vodacom Miss Tanzania 2010 wakizungumza na mmoja wa vijana wanaojishughulisha na kazi ya kusindikiza watalii kupanda Mlima Kilimanjaro leo mchana wakati warembo hao walipotembelea Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA) iliyopo Marangu mkoa wa Kilimanjaro. Warembo 30 wa Vodacom Miss Tanzania wapo katika ziara ya kuhamasisha utalii wa ndani katika mikoa ya Kanda ya Kaskazini.

Warembo hao wakiingia katika Viwanja vya Hifadhi ya KINAPA wakiwa mabegi yao mgongoni..

Mhifadhi katika Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA), David Loosurutia (kushoto) akitoa ufafanuzi juu ya mazingira ya hifadhi hiyo kwa warembo wa Vodacom Miss Tanzania 2010 wakati warembo hao walipotembelhi hiyo leo mchana.

Baadhi ya warembo wa Vodacom Miss Tanzania 2010 wakiangalia michoro ya ramani ya Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kialimanjaro (KINAPA) wakati warembo hao walipotembelea hifadhi hiyo leo mchana. Jumla ya Warembo 30 wa Vodacom Miss Tanzania wapo katika ziara ya kuhamasisha utalii wa ndani katika mikoa ya Kanda ya Kaskazini.
No comments:
Post a Comment