Na Mwandishi Wetu, Arusha
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema, Dk. Wilbroad Slaa, amesema kuwa hayuko tayari kukaa meza moja na serikali ya kihuni, iliyompa barua na baraka ya kufanya maandamano ya amani na mkutano na baadaye kutuma askari kupiga wananchi na kumwaga mabomu ya machozi hatimaye kusababisha vifo. Dk Slaa aliyasema hayo jana, wakati alipokuwa katika hospitali ya Mkoa Mount Meru, akiwajulia hali majeruhi waliojeruhiwa kwa risasi na Polisi, waliotumia mabomu ya machozi, maji ya kuwasha na risasi za moto, kuwatawanya katika maandamano ya mkutano wao wa hadhara wa NMC, uliofanyika Januari 5 mwaka huu. Dk. Slaa alisema kuwa katika kuhakikisha chama chake kinatumia Demokrasia ya kweli na haki ya kikatiba, Desemba 22 mwaka jana 2010, iliandika barua kwenda kwa msajili wa vyama vya Siasa, John Tendwa, ya kumweleza juu ya kutaka kufanya mazungumzo kufikia muafaka wa Arusha na kumweleza ifikapo Januari 4 kama hakuna mazungumzo wataitisha maandamano na mkutano. “Pamoja na kuandika brua hiyo, bado ilipofika januari 3 mwaka huu, majira ya saa 10 za jioni, Mimi Slaa nilimpigia simu Tendwa kumuuliza vipi muafaka ukoje akasema anamtafuta IGP na Waziri wa TAMISEMI kubaini nini kinaendelea na atampatia jibu ” alisema Dk. Slaa. Alisema kuwa baada ya hapo kweli Tendwa alimpigia simu na kumtaka Dk. Slaa kuendelea na maandamano na mkutano wake, baada ya kumpigia simu mara nne na simu ya mwisho alipokea saa 3.00 usiku na kuagana. Aidha alisema wakati wakijadiliana na simu, Tendwa alimuuliza Dk. Slaa amtajie ajenda anazotaka amtajie za kuongea naye katika mkutano watakaokaa na Dk. Slaa alisema hawezi kutaja kwenye simu, bali wakutane kwenye kikao na wazitaje na kukubaliana nazo, kasha wakaagana. “Hayo yalikuwa mazungumzo ya Januari 3 mwaka huu na januari 4 majira ya saa 6.00 mchana nikaondoka Dar na kuanza safari kuja Arusha, kwa ajili ya maandamano na mkutano, ila nikiwa njiani majira ya saa 8 mchana, Tendwa alinipigia simu niko wapi na nikamjibu niko Kibaha, Tendwa akaniambia je tukitangaza uchaguzi wa Meya Arusha, Mwanza na Kigoma, hlafu msifanye mkutano sawa” akaniuliza” alisema Dk. Slaa. Alisema baada ya kumuuliza swali hilo, Dk. Slaa alimjibu kuwa, hawezi kufuta maandamano na mkutano, kwa sababu tayari siku imefika na wametumia dharama nyingi kuutangaza, hivyo akashauri, wafanye mkutano wao na wakimaliza wakutane kwa kikao kw aajenda hiyo. Alisema baada ya kumjibu hivyo Tendwa alimkubalia na kukata simu, lakini ilipofika saa 10 za jioni siku hiyo ya taree 4 januari, Tendwa akampigia simu na kumweleza kuwa ametumka barua ofisi za Chadema na alipomuuliza sekritari wake akakiri kupokea barua ya kutoka kwa msajiri wa vyama vya siasa. “Nikamwambia Sekritari anisomee barua hiyo, kw akuw anipo njiani, japo nilikuwa naogea naye kwa simu kila wakati, akanisomea, ambapo sehemu ya barua hiyo ilianza kwa kuomba radhi kw akutokutana Desemba 22 kama walivyokubalina naye” alisema Dk. Slaa kwa kunukuu sehemu ya barua hiyo. Pia alisema barua hiyo ilisema kuwa Tendwa na Waziri Mkuu kwa pamoja wamekubalina wafanye mkutano wa kupanga ajenda na mwisho alimtaka Dk. Slaa afanye maandamano na mkutano wake bila kutumia lugha ya kashfa na kutumia lugha za kistaarabu, kwa kuwa tayari suala la Meya Arusha na Majiji mengine watatatua. “Mimi nilipomaliza kusomewa barua hiyo, nikampigia Msajili na kumuuliza kuwa, kama yeye ni mwanasheria, anieleze lugha ya kashfa tafsiri yake ni nini, ila Tendwa akacheka, nikamuuliza wewe umekuwa Mahakama una weza kutafsiri sheria kuwa hii ni lugha ya kashfa, maana Mahakama ndiyo yenye kujuwa kama kuna kashfa au la kwa kutafsiri sheria, Tendwa akacheka na kunitakia mkutano na maandamano mema, tukaachana kwa simu” alisema Dk. Slaa. Alisema ilipofika saa 12 jioni, siku hiyo ya Januari 4, tendwa alimpigia Dk Slaa simu na kumtaka asifanye mkutano wala maandamano, kwa sababu anamtafuta Mkuchika kwa ajili ya mazungumzo. “Mimi nikamwambia hataweza kubadili msimamo wake lazima afanye mkutano, akamtakia kila la heri, nay eye akalazimika kulala njiani kabla ya kufika Arusha na Januari 5 aliiingia Arusha na kupokelewa na wafuasi wa chama chao Phillips hadi Mount Meru Hotel” alisema Dk. Slaa. Alisema baada ya kukutana hapo kwa muda, walishaurina na Phillimon Ndesamburo, kupanda magari na kuelekea viwanja vya NMC ili kupokea maandamano hayo na wakafanya hivyo, huku wenzao akina Mbowe na viongozi wengine wenye nguvu za kuandamana waliaandamana. “ lakini nilipofika viwanja vya NMC, Polisi waliingia na kuanza kupiga mabomu, na kunilazimu kushuka jukwaani na wafuasi wa chadema wakaniletea maji kunawa usoni ili kupunguza makali ya mabomu na kasha nikapanda jukwaani tena kuuliza askari kwa nini wanapiga watu mabomu na mkutano una kibari, hawakujibu” alisema Dk. Slaa. Akiwa anahutubia akaambiwa viongozi waliokuwa wanaandamana wamekamatwa na wamewekwa ndani, ndipo akashangaa kwa nini wafanye hivyo na kuwataka wawaachie viongozi hao kwa kuwa walikuwa wanatimiza haki ya kikatiba na wana kibali. “Pia lazima FFU wakitaka kuzuia mkutano, sheria inasema ni lazima watoe tangazo mara tatu kwa kutumia kipasa sauti kikubwa na anayetangaza awe Ofisa wa Jeshi la polisi, lakini kwa Arusha hawakufanya hivyo, waliamua kuchakachua sheria kila kitu na kutumia Dola vibaya” alisema Dk. Slaa. Alisema kutokana na hali hiyo hawezi kupokea barua toka serikalini, kupitia kwa Msajili wa vyama vya Siasa na nyingine Polisi Arusha kuwaruhusu kufanya maandamano na mkutano, kasha kuwapiga mabomu na kuwatoa damu na kusababisha vifo watu wasio na hatia. “Sasa nitajadiliana nini na serikali ya kihuni namna hii, ambayo inatoa barua na kuzichakachua juu kw ajuu bila kufuata sheria walizonanazo wenyewe” alihoji Dk. Slaa. Hata hivyo kwa upande wa Majeruhi anasema kama chama wamejipanga kuwasaidia na ata zile familia zilizopoteza watu wao, wanafanya tathimini ili waweze kutoa tamko, pamoja na kueleza idadi kamili ya vifo, maana vilivyoripotiwa kuwa vimechakachuliw ana idadi hiyo hailingani na hali halisi.
|
No comments:
Post a Comment