TIMU ya Simba ya Jijini Dar es Salaam, leo imeibuka na pointi tatu muhimu kwenye Uwanja wa Taifa dhidi ya Mtibwa Sugar ikiwa na Kocha mpya Jackson Mayanja aliyekabidhiwa timu hivi majuzi baada ya kutimuliwa aliyekuwa Kocha Mkuu wa Club hiyo, Dylan Kerr. 
Simba imeibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa mapema katika dakika ya Nne ya kipindi cha kwanza kupitia kwa  mshambuliaji Hamisi Kiiza.
Pamoja na ushindi huo Simba bado wamebaki nafasi ya tatukatika msimamo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, wakiwa na pointi 30 sawa na Yanga inayoshika nafasi ya pili, lakini Yanga wakiwa mbele kutokana na kuwa na mabao mengi ya kufunga.
Hiyo ni mara ya pili kwa Simba na Mtibwa kukutana katika kipindi cha wiki mbili kwani walikutana kwenye mchezo wa nusu fainali wa kombe la Mapinduzi na Mtibwa Sugar kuibuka na ushindi wa bao 1-0.
Nao Azam Fc leo wameshikwa shati na African Sports wakiwa kwenye Uwanja wao wa nyumbani baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1.
Bao la Azam Fc lilifungwa na Kiungo Frank Domayo katika dakika ya 28 kipindi cha kwanza na bao la kusawazisha likifungwa na Hamadi Mumba dakika 59
MATOKEO MENGINE YA LIGI KUU MICHEZO YA LEO NI KAMA IFUATAVYO:-
| JKT Ruvu | 1 - 5 | Mgambo JKT | |
| Toto Africans | 0 - 1 | Tanzania Prisons | |
| Simba SC | 1 - 0 | Mtibwa Sugar | |
| Stand United | 1 - 0 | Kagera Sugar | |
| Mbeya City | 1 - 0 | Mwadui FC | |
| Coastal Union | 1 - 1 | Majimaji | 
KESHO Januari 17, 2016
Yanga SC Vs Ndanda FC, Uwanja wa Taif
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
No comments:
Post a Comment