Habari za Punde

*WADAU WAKUTANA KUJADILI NJIA MAHUSUSI ZA KUBORESHA MAZINGIRA NA KUKABILIANA NA ATHARI ZA MABADILIKO YA TABIANCHI KWE MAJIJI

Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu Rais, Ngosi Mwihava akifungua mkutano huo wa wadau ambao umewashirikisha pia watendaji wa serikali na mashirika yasiyo ya serikali kutoka katika wizara na idara mbalimbali,  kwa lengo la kujadili kwa pamoja namna ya kushirikiana na kupata njia ya pamoja ya kuboresha mazingira na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi zikiwemo mafuriko, magonjwa na uharibifu wa miundombinu.

Wadau wa mazingira kutoka idara na wizara mbalimbali za serikali na mashirika binafsi wamekutana Januari 20, 2016 kujadili njia mahususi za kuboresha mazingira na kukabilaiana na athari za mabadiliko ya tabianchi kwenye majiji

Majadiliano hayo ni hatua moja wapo ya uanzishwaji wa mfuko wa Mfuko wa Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi ukiwa na lengo la kukusanya pesa za kukabiliana na changamoto za mazingira na mabadiliko ya tabianchi katika Manispaa ya Ilala

Mradi huo unafanywa kwa ushirikiano wa Manispaa ya ilala na ForumCC
Wadau wakifuatilia Mkutano huo. KUSOMA ZAIDI BOFYA READ MORE
Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu Rais, Ngosi Mwihava (katikati) akiwa na viongozi wa Forumcc wakati wa mkutano huo, kuanzia kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi anayeshughulikia Mabadiliko ya Tabianchi katika Ofisi ya Makamu wa Rais, Richard Muyungi, Mkurugenzi wa Mazingira katika Ofisi ya Makamu wa Rais, Julius Ningu wakati kuanzia kulia ni Afisa Miradi Forumcc, Fazal Issa na Mwenyekiti wa bodi ya forumcc, Yusta Kibona
Mkurugenzi wa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, Dr. Julius Ningu akifafanua jambo wakati wamkutano huo
Meneja Miradi Forumcc, Rebecca Muna akielezea jambo wakati wa mkutano huo
 Picha ya pamoja
Profesa Robert Kiunsi kutoka Chuo cha Ardhi akiwasilishwa mada kuhusu atharai za mabadiliko ya tabianchi na namna ya kubabiliana na athari hizo
Amy Faust Kutoka Benk ya Dunia akiwasilisha mada ya mifano ya miradi ya kuboresha mazingira katika majiji ilivyofanikiwa katika nchi nyingine huko Ulaya, mifano ambayo inaweza kutumiwa pia hapa nchini
Francis Gowele, Afisa Mazingira Manispaa ya Ilala akitoa report ya mazingira katika manispaa hiyo
Mwezeshaji wa mkutano huo Abdallah Henku akielezea jambo wakati wa mkutano huo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.