HATIMAYE Mahasimu wawili na watani wa jadi katika soka la Bongo timu za Yanga na Simba wamekutana katika hatua ya Nusu Fainali kwenye Mashindano ya Kombe la Mapinduzi yanayoendelea mjini Zanzibar.
Yanga anacheza na Simba keshokutwa Jumanne usiku baada ya kufungwa na Azam fc katika kundi lao kwa jumla ya mabao 4-0 katika mchezo uliopigwa jana usiku na kushika nafasi ya pili wakiwa na Pointi 6 na mabao 8, huku Azam Fc wakifikisha Pointi 7 na mabao 5 na kuongoza kundi B.
Nao Simba wameweza kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Jang’ombe Boys katika mchezo uliopigwa jioni ya leo kwenye uwanja wa Aman Mjini Zanzibar ukiwa ni mchezo wa mwisho wa Kundi A.
Simba imemaliza mechi zake ikiwa na jumla ya Pointi 10 ikiongoza Kundi A ikifuatiwa na Taifa jang’ombe ikiwa na pointi tisa, Jang’ombe Boys, ikiwa na Pointi sita na URA yenye pointi nne.
No comments:
Post a Comment